SAVINHO X DOKU✍🏻Wingers wawili ambao wana kasi , wanaweza kukota mpira vizuri tena kwa kasi , wanajua kudumisha mapana ya uwanja kusaidia timu yao kushambulia vizuri ( kuwafanya wapinzani kuzuia eneo kubwa la uwanja ) , umri upo upande wao bado LAKINI SASA :-1: Bado ile decision making inawasumbua : Nini wanatakiwa kufanya katika wakati gani2: Final Product : wanaweza kufanya vitu vingi kwa usahihi lakini katika kumalizia kitendo cha mwisho bado hawajafika katika level ambayo Pep naamini anaitaka3: INCONSISTENCY : Hawana bado muendelezo mzuri wa viwango vyao tena kwa bahati mbaya sio mechi kwa mechi tu bali ndani ya mechi moja unaweza kuona dakika 10 anacheza vizuri sana halafu dakika 5 zinazokuja unashangaa huyu ni pacha wake ?Kwa staili ya football ya Pep Guardiola wingers ni watu muhimu sana katika kufanya timu yake icheze kwa ufanisi zaidi : Hao wawili ( Doku na Savinho ) nafikiri wapo kwenye muda wa mkopo , nikimaanisha wanahitajika kuboresha haraka vinginevyo Pep huwa mara chache sana huwa anasubiria mtu 😀BRIGHTONBaada ya kuchukua WIKI ( 7-0 ) kutoka kwa Notts Forest wamecheza jumla ya mechi 7 mfululizo ( pamoja na leo ) bila kupoteza✍🏻Nne wameshinda EPL na moja sare na mbili wameshinda za FA Cup . Hii ndio tunaita kurejea kwenye ubora baada ya kuvurumishwa . Bado rada yao ipo kwenye kucheza UCL msimu ujao✍🏻Kumbuka msimu ujao EPL wana nafasi ya timu 5 kucheza UCL yani namba moja mpaka namba tano .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here